RAIA WA JIMBWE WAOMBA MSAA BAADA YA KUKIMBIA VITA

Gepubliceerd op 28 mei 2023 om 19:39

Nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo katika Jimbo la Tanganyika mara kadhaa hali ya migogoro ya ukabila inasababisha watu kuhama makaazi Yao. Vita baina ya makabila ya watwa na Bantu ni Moja ya vita inayoendelea katika Jimbo hilo ambalo lina watu zaidi ya milioni Tatu. Umoja Radio ilitembelea Kijiji Cha Jimbwe kilichopo umbali wa kilomita zaidi ya 20 kutoka Kalemie na kuwakuta baadhi ya raia walio kumbana na mikasa ya kukimbia ugomvi wa vita vya ukabilaRaia hao wa kabila ya watwa ambao walihama sehemu hiyo hapo awali kufuatana na mapigano ya ukabila na kurejea kwenye maeneo Yao ya asili wamesema maisha Yao ni magumu huku wakidai ukosefu wa chakula ni Moja ya matatizo wanayokabiliana nayo huku wakiomba kwa serikali na mtu anayeweza kuwasaidia awaangalie kwa jicho la Tatu Ili wapate chakula.

Wakiongea na Umoja Radio wakaaji hao Wamesema kuwa njaa, masomo, hospitali ni vitu vinavyowasumbua. Upande wa chakula wanaomba msaada kwa mtu, shirika au serikali kuwasaidia Ili wapate kulisha watoto.Watoto wanashindwa kuhimili njaa hadi inawapelekea kuumwa na mara kadhaa wanapoteza maishaRaia hao waliongeza kuwa watoto wanatembea kilomita 7 kwenda sehemu yalipo masomo na hospitali, upande wa hospitali wamesema ni shida kwao pale mwanamke anapotaka kuzaa inawapa tabu kufikia hospitali. Wanatoa wito wa kusaidiwa. Wakimalizia kuongea na Umoja radio, watu hao wamesema kuwa wao pia ni raia wa Kongo na wanaitaji Kongo kuwa na mshikamano

 

 

Reactie plaatsen

Reacties

Er zijn geen reacties geplaatst.