Kombe la Dunia la 2026: muundo mpya wa mchujo uliopitishwa Afrika
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) linatangaza kuwa litaandaa droo rasmi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la FIFA la 2026 kwa vyama wanachama wake mnamo Julai 12 huko Cotonou (Benin), siku moja kabla ya mkutano wake Mkuu wa 45 wa Kawaida. Tangazo hili lilitolewa Alhamisi hii, Mei 18 mwishoni mwa kikao cha kamati ya utendaji ya shirikisho la soka barani Afrika, kilichokutana mjini Algiers (Algeria) chini ya uongozi wa rais wake, Patrice Motsepé wa Afrika Kusini. Katika mkutano huu, CAF ilionyesha kuwa imeidhinisha muundo na tarehe za mechi hizi za mchujo. "Muundo mpya umebadilishwa kwa muundo uliopanuliwa wa Kombe la Dunia la FIFA na utahusisha vyama vya wanachama 54 vya CAF ambavyo vitagawanywa katika vikundi tisa (9)," taarifa kutoka CAF ilisema.