Bunge la jimbo la Tanganyika lapiga kura kumtoa gavana

Gepubliceerd op 18 mei 2023 om 19:05

Bunge la Jimbo la Tanganyika limepiga kura ya kutokuwa na Imani na Gavana wa Jimbo hilo Julie Ngungwa Mwayuma.

Hayo yametokea baada ya mbunge KAKUDJI NGOY Kuandika kibarua ili Gavana afike bungeni kujibu maswali kuusu ubadhirifu wa fedha ambazo hazijulikani zimetumikaje.

Wabunge 14 kati ya 25 walijitokeza bungeni n’a kupiga kura ya kutokuwa na Imani na gavana, kura ambazo zinawapa wabunge uzito na kusababisha Gavana kuachia madaraka.

Julie Ngungwa Mwayuma hajatokea bungeni baada ya kupendekeza kikao hicho kifanyike tarehe 08 mei 2023 kwasababu alikua anaenda kufuatilia matibabu. Jambo ambalo bunge limesema ni kuizarau bunge hilo. Duru zinazoaminika zinasema kuwa Gavana bado yupo mjini Kinshasa

Reactie plaatsen

Reacties

Er zijn geen reacties geplaatst.